Historia Fupi
Shule inamilikiwa na JESHI LA MAGEREZA na ilianzishwa mwaka 1978 ikiitwa Ubena Sekondari ili kutoa elimu ya Sekondari kwa Askari wa Gereza la Mifugo Ubena ambalo lilikuwa maalum kwa wafungwa waliokuwa Watumishi wa Serikali ambao kiwango chao cha elimu kilikuwa cha juu ukilinganisha na Askari wengi wa kituo hicho. Kilianza kama kituo cha maandalizi ili kufanya mtihani wa kidato cha nne.
Mwaka 1981 Shule ilianza kupokea wanafunzi wa maeneo ya jirani na Shule. Shule ilisajiliwa kwa namba P.170 ikaanza kupokea Askari wa vituo vyote vya Magereza walioajiriwa wakiwa na elimu ya darasa la saba. Lengo lilikuwa kuwapatia elimu ya Sekondari kama matakwa ya mfumo wa ajira Serikalini kuwa lazima kila mtumishi awe na elimu ya Sekondari. Mwaka 2000 Shule ilisajiliwa na kupata namba S.1264 na kuitwa Bwawani Sekondari na kuanza kupokea wanafunzi waliomaliza darasa la saba toka kwa wanajamii wote wa Kitanzania wakiwemo jamii za kiaskari na kiraia. Ni shule ya bweni na kutwa kwa wanafunzi wa kike na kiume.
Shule Ilipo
Shule ipo eneo la Bwawani-Visakazi, Barabara ya Dar-es-Salaam -Morogoro . Halmashauri ya Wilaya Chalinze, Kata ya Ubena Zomozi, barabara kuu iendayo Morogoro, km 39 kutoka Chalinze kuelekea Morogoro na km 49 kutoka Morogoro kuelekea Dar-es-Salaam.
Mafanikio ya shule
Uwezo na historia nzuri ya shule ilipelekea kusajiliwa kufundisha masomo ya kidato cha Tano na Sita katika michepuo ya Sayansi na Sanaa. Aidha ufaulu wa Shule umekuwa ukipanda mwaka hadi mwaka.
Imeshatoa wanafunzi wengi kujiunga na kidato cha Tano toka kuanzishwa kwake.
Imeshatoa wanafunzi wengi kusoma fani mbalimbali ndani na je ya nchi.
Imeshachangia kupatikana kwa wataalamu katika fani mbalimbali ambao wanafanya kazi kwa ufanisi katika Taasisi mbalimbali nchini.
We value the importance of supporting learning and bringing out the absolute best academic success in every student. Come and visit us and experience it for yourself. We work to ensure our students have opportunities to learn in a 21st century way. They are challenged to think for themselves, to work co-operatively in teams and to articulate their ideas fluently. Students are also expected to master the core knowledge required for each subject, but this is certainly not achieved by a chalk and talk methodology. The focus in lessons is on understanding concepts and students actively applying their learning.
Your child deserve the best education at a top school. We are committed to enabling a wide range of families to access our school and offer very reasonable fees. We aim to inspire all our children to reach new heights. They will receive the finest education, and it will be clear to all they meet that they have developed a contemporary world view, are respectful, kind and committed.
Learning with us will open doors for your children’s futures.